Kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) Meja Jenerali Ali Ja'fari amesema:Iran haitishiki na vitisho vya Marekani kuivamia iran kijeshi,
kupambana na Marekani ni fursa ambayo tumekuwa tukiitamani na kuisubiri kwa muda mrefu sana, Marekani inapaswa ifahamu kwamba, jeshi letu limejiandaa kwa muda mrefu sana kwa ajili kupambana na Marekani, na kwamba Marekani ifahamu kwamba vita kati ya Marekani na Iran ni kitu ambacho kinasubiriwa na kutamaniwa na waumini na wanamapinduzi duniani kote,wanajeshi na wanamapinduzi wetu wanaisubiri sana siku mtakayo jidanganya kuivamia Iran ili waweze kuonyesha ujuzi wao.
Haya ni majibu yaliyotelewa na kamanda wa Iran baada ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani kutishia kuivamia Iran kijeshi.